Wednesday 30 August 2017

RASIMU PENDEKEZWA YA KATIBA - ASILI YETU ( YETU FOUNDATION )



ASILI YETU – YETU FOUNDATION- 2017
KATIBA YA KIKUNDI – ASILI YETU
(YETU FOUNDATION)
KIKUNDI CHA VIJANA NDANI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MKOA WA MBEYA
2017

“Ulipo Tupo”



                                    KATIBA YA ASILI YETU – ASILI YETU FOUNDATION.
YALIYOMO:
Contents






















SEHEMU YA I:  UTANGULIZI

IBARA YA 1: JINA LA KATIBA, KAULI MBIU NA KUANZA KUTUMIKA

1.1  Katiba hii itajulikana KamaKATIBA YA ASILI YETU -2017.

1.2  Kauli mbiu ya Chama Cha Asili Yetu ni : Ulipo tupo
1.3. Katiba hii imepitishwa Kwa kauli moja na wanachama katika Mkutano Mkuu.

IBARA YA 2: TAFSIRI YA MANENO

2.1 ASILI: Chanzo na halisia ya kilichopo na Kilichoundwa katika miliki ya Mwana-Adam.
2.2YETU: Miliki (kilichoonekana na Kisichoonekana)katika mazingira Ya Mwana-Adamu.
2.3 FOUNDATION: Tafsiri ya lugha ya Kiingereza yenye maana ASILI.
TAFSIRI  ZAIDI
a.Kikundi” lina maana ya Kikundi cha ASILI YETU (YETU FOUNDATION)
b. “Mwanakikundi”  ni  mtu  yeyote  aliyejiunga  na  kikundi  na  anayeshiriki  kikamilifu  kutimiza kanuni na taratibu za kikundi.
c.”Viongozi”ni  wanakikundi  waliochaguliwa  au  kuteuliwa  kwa mujibu  wa  katiba  hii au kanuni za kikundi, kusimamia mali au uendeshaji wa shughuli yoyote ya kikundi.
d.“Mtoto” ni mtu mwenye umri chini ya miaka 18.
e. “Kitega uchumi”(Investment)ni uwekezajiwenye kuleta tijakwa kikundi
f. “Kanuni”  za  kikundi  ni  taratibu zote  zilizopitishwa  na  wanakikundi  kutumika  kwenye kikundi katika kuitekeleza katiba hii na kufanikisha madhumuni/malengo ya kikundi.
g. “Ndani  ya  Tanzainia”  Ndani  ya  nchi  ni  mipakaambayo  kijiografia inahusisha maeneo  yote ndani  ya  jamhuri  ya  muungana  na  nje ya  nchi  itamaanisha  maeneo yote  yasiyokuwa  ya Tanzania
h. “Mkutano  halali”   ni  kikao  chochote  au  mkutano  wowote  wa  wanachama
ulioitishwa kulingana na katibahii au kanuni za kikundi na uliofanywa kwa utaratibi uliowekwa




2.4   AINA  YA KIKUNDI
ASILI YETU ni Kikundi cha Kijamii cha Kimaendeleo ya Kiuchumi (Community Based Organisation - CBO)

SEHEMU YA II: KATIBA, USAJILI, OFISI KUU NA ENEO LA UTENDAJI

IBARA YA 3: Katiba ya kikundi cha Vijana wenye lengo la kuleta mabadiliko chanya katika fikra Na matendo yenye Kuakisi Uzalendo Nauhalisia.
IBARA YA 4:  Jina la Kikundi litakuwa ASILI YETUNa kita tambulika KamaAY.
IBARA YA 5: Usajili: Kikundi hiki kitakuwa chini ya sheria na.337 ya mwaka 2002 Na kitakuwa Kikundi cha hiari.
IBARA YA 6:Ofisi kuu ya kikundi itakuwa MBEYA, Mbeya Mjini, kata Ya Iganzo/Isanga Mtaa wa AsiliKama ilivyoamuliwa na Mkutano Mkuu wa Kikundi.  Pia zinaweza kuanzishwa ofisi ndogo za kikundi Kwa kadiri itakavyoonekana Na mkutano mkuu kuwa inafaa kuwa Na ofisi hizo
IBARA YA 7: Eneo la Utendaji kazi litakuwa eneo lote la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hususani Mkoa wa Mbeya, Mbeya Mjini.
IBARA YA 8:  Katiba hii inatoa nafasi ya kuwa na kanuni za Maadili kwa wanakikundi na Viongozi.

SEHEMU YA III: DIRA, DHAMIRA NA MADHUMUNI

IBARA YA 9:  Kauli Dira ya ASILI YETU itakuwa: Kuwa Kikundi pekee cha Kusaidina, kuungana na kunufahisha wanakikundi Na jamii yake.
IBARA YA 10: Kauli ya Damira: Kuanzisha Na kutunza misingi ya ushiriki wa pamoja katika utendaji na uanzishwaji wa shughuli za manufaa ya wanakikundi na jamii.
IBARA YA 11: Madhumuni ya Kikundi ya takuwa Kama ifuatavyo;
A: LENGO KUU
Kushirikiana kijamii Na kiuchumi
B: MALENGO MAHUSUSI
(a)    Kushirikiana na kusaidiana wakati wa shida na raha

(b)   Kuwezesha wanakikundi kuimarishana kiuchumi na hali ya maisha kwa:

-i. Kupokea na kuweka michango ya fedha za wanakikundi
ii. Kuanzisha Na kuendeleza shughuli zozote halali za kiuchumi kwa manufaa ya wanakikundi kama itakavyokubaliwa katika mkutano halali wa wanakikundi
iii.    Kuwezesha kifedha shughuli binafsi za wanakikundi kwa masharti yaliyokubaliwa na wanakikundi
iv.     Kuhamasisha ushirikiano na wanakikundi wenye changamoto mbalimbali kama ulemavu,

v. Kushirikiana Na uongozi wa Serikali na Idara mbalimbali katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya Jamaii kama itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu.
vi. Kusaidia wanakikundi wake Na jamii zao Kwa lengo la kustawisha na kuboresha maisha yao.
Vii. Kuanzisha Na kushiriki shughuli za kiuchumi Kama vile miradi ya kimaendeleo ambayo itasimamiwa Na wanakikundi.
viii. Kuanzisha na kushiriki kuboresha huduma za jamii kama elimu, afya, mazingira ,Uchumi na Michezo.
ix. Kufanya shughuli nyingine yoyote isiyopingana Na sheria ambayo Jamii na mkutano mkuu utaridhia kuwa ifanyike.

SEHEMU YA IV: UANACHAMA, AINA ZA WANACHAMA NA KURUDISHIWA

UANACHAMA

IBARA YA 12:UANACHAMA

12.0. Kutakuwa na aina mbili zifuatazo za uanachama ambazo ni;

12.1.     Mwanachama wa Kawaida
Ni mtu yeyote yule ambaye ametimiza taratibu zote za kujiunga Na Kikundi au Umoja huu Kwa mujibu wa Katiba na Kanuni zake ikiwa ni pamoja na kulipa Ada na Michango stahiki.
12.2.     Mwanachama wa Kutunukiwa
Mwanachama wa Kutunukiwa ni Mtu yeyote atakaetunukiwa uanachama kupitia maamuzi au azimio la Mkutano Mkuu katika kuthamini Mchango uliotolewa na Mtu huyo ama atakaoendelea kuutoa kwa kuleta maendeleo na ufanisi wa Malengo ya Kikundi au Umoja huu.
12.2.1           Sifa za kuwa Mwanachama
(i)                 Awe na Umri usiopungua miaka 18.
(ii)               Awe mwenye nia na awe tayari kuwa mwanachama
(iii)             Awe tayari kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kikundi
(iv)             Awe na akili timamu.
(v)               Awe tayari kutii na kufuata masharti ambayo yameainishwa kwenye Katiba na Kanuni za kikundi
(vi)             Awe tayari kulipa kiingilio pamoja na ada ya uanachama ya kila mwezi
12.3.1      Haki za Mwanachama
(i)     Kutoa maoni yake kwa uhuru
(ii) Kuchagua au kuchaguliwa katika nafasi yoyote ile ya Uongozi katika Kikundi au Umoja huu.
(iii)         Kuwasiliana Na Uongozi/Viongozi ikiwa ni pamoja na kupokea na kutoa taarifa zinazohusu Kikundi au Umoja huu.
(iv)          Kuhudhuria na/au kuwakilisha katika jambo lolote lile linalohusu Kikundi au Umoja huu Kwa kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba hii.
(v)  Kupewa nafasi ya kujieleza na kujitetea pindi anapokabiliwa na tuhuma zozote zile dhidi yake katika umoja huu.
(vi)          Kutumia Mali za Kikundi kwa kufuata utaratibu na Kanuni za Umoja huu.
(vii)       Ana haki ya kutoa hoja yake na kusikilizwa wakati wa kushiriki majadiliano kwenye vikao.
(viii)     Kufahamu mapato na matumizi ya Kikundi kwa kutumia na kuzingatia Kanuni.
(ix)          Kusaidiwa linapomtokea tatizo.
(x)   Kusaidiwa kimawazo au kiuchumi kulingana na hali itakavyo ruhusu.
12.3.2           Wajibu wa Mwanachama.
(i)                 Kuilinda na kuitetea katiba hii wakati wote.
(ii)               Kutekeleza majukumu atakayopewa na viongozi au wanachama wenzake.
(iii)             Kushiriki katika shughuli zote za kikundi kwa mujibu wa katiba hii ikiwa ni pamoja na vikao halali vya Umoja huu.
(iv)             Kulipa ada pamoja na michango mbalimbali itakayo pitishwa na Kikundi au Umoja  huu.
(v)               Kueneza sifa nzuri za Umoja huu.
(vi)             Kutii na kufuata maagizo na maazimio ya Mkutano/Mikutano halali ya Umoja huu, hata ikiwa hatakuwepo kwenye Mkutano huo, au hakushiriki katika kupitisha azimio hilo.
(vii)           Kuwa na nidhamu wakati wa Mikutano ama shuhuli nyingine zozote za Kikundi.
(viii)         Kutunza siri zote za Umoja huu
12.3.3             Kujiunga na Kikundi.
i.    Kujaza Fomu ya maombi itakayotolewa kwa ada itakayokuwa imepangwa.
Maombi haya ni lazima yapitiwe na kukubaliwa na Uongozi, kisha kupitishwa na MkutanoMkuu au Mkutano Mkuu Maalum.
ii.           Baada ya kukubaliwa Mwombaji atatakiwa kulipa Ada ya kiingilio cha kiasi kitakachokuwa kimepangwa na Mkutano Mkuu au Mkutano Mkuu Maalum kwa wakati huo.
iii. Pamoja na Ada ya kiingilio Mwanachama mpya atalazimika kulipa Mchango wa Miezi Miwili au zaidi Ili aweze kuwa Mwanachama kamili wa Kikundi.
iv. Awe tayari kulipa kiingilio pamoja na ada ya uanachama ya kila mwezi
IBARA YA 13: KUKOMA UANAKIKUNDI,
i.          Mwanakikundi akifariki.
ii.         Mwanakikundi akijiuzulu Kwa hiari yake.
iii.       Akishindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila kutoa taarifa yenye kuelezea sababu zinazoridhisha Kwa kushindwa kwake kuhudhuria.
iv.       Akishindwa kulipa ada ya miezi sita au Kama ana madeni sugu kwenye kikundi au miradi ya kikundi.
v.        Kufukuzwa uanakikundi kutokana na kuthibitika kuwa.
a.       Mwakakikundi Kafanya kazi binafsi kwa kutumia jina la kikundi bila kikundi kuwa na taarifa.
b.      Kufanya udanganyifu au kujipatia fedha za kikundi isivyo halali.
c.       Kwa kukosa maadili na kuvunja katiba hii pamoja na miongozo mingine ya kikundi kwa makusudi
vi.       Mwanakikundi aliyefukuzwa Kama ilivyoelezwa hapo juu (v) hatarudishiwa fedha za ada, kiingilio na michango ya aina nyingine isipokuwa fedha zitokanazo na miradi aliyoshiriki kwa kadiri itakavyokuwa imeamuliwa na kikundi.
IBARA YA 14: MAJUKUMU YA MWANAKIKUNDI YATAKUWA YAFUATAYO;
i.                Kuhudhuria vikao vyote vya kawaida Na vya dharura.
ii.               Kushiriki katika shughuli za wanakikundi ambazo zitaamuliwa na mkutano wa wanakikundi.
iii.             Kulipa ada ya kiingilio na ada ya mwezi pamoja  michango mbalimbali itakayoidhinishwa na kikundi.
iv.             Kuheshimu, kusimamia na kuzingatia katiba hii.
v.              Kuwa na nidhamu katika mikutano, vikao na katika shughuli za Kikundi.
vi.             Kuchagua viongozi wa kikundi kwa kadiri ya miongozi ya kikundi.
vii.           Kufuata taratibu zilizowekwa na katiba ya kikundi au kanuni zake.

IBARA YA 15: Kurudi Kwa mwanakikundi aliyeachishwa
i.          Mwanakikundi aliyeachishwa uanachama au kujitoa ataweza kurudi ikiwa tu itathibitika kuwa amemaliza tatizo lililofanya uanachama wake ukome  au ameomba radhi kwa kosa lililompelekea uanachama wake kusitishwa.
ii.         Mwanachama  anayeomba  kurudishwa kundini baada ya uanachama wake kusitishwa atapaswa kujaza fomu mpya ya maombi sawa na mwananachama mpya na  atatakiwa kulipa ada zote tangu tarehe ya kuachishwa  uanachama.
iii.       Muda wake wa uanachama utatahesabiwa kuanzia aliporejeshwa kuwa mwanachama.

SEHEMU YA V: MUUNDO WA UONGOZI

IBARA YA 16:  Kikundi kitakuwa na Uongozi ufuatao
1.    Mwenyekiti.
2.    Katibu.
3.    Mwek hazina
IBARA YA 17:  SIFA ZA MWENYEKITI;
i.          Awe Na sifa zote za mwanakikundi wa kawaida.
ii.         Awe mwanakikundi Kwa muda wa miaka mitatu (3) mfululizo isipokuwa viongozi wa kwanza kuchaguliwa baada ya usajili wa katiba hii hawatafungwa na sharti hili la muda.
iii.       Asiwe amepatikana Na hatia ya kosa lolote la jinai.
IBARA YA 18: SIFA ZA KATIBU
i.          Awe Na sifa zote za mwanakikundi wa kawaida.
ii.         Awe mwanachama Kwa muda wa miaka mitatu (3) mfululizo isipokuwa viongozi wa kwanza kuchaguliwa baada ya usajili wa katiba hii hawatafungwa na sharti hili la muda.
iii.       Asiwe amepatikana na hatia ya kosa lolote la jinai.
IBARA YA 19: SIFA ZA MWEKA HAZINA
i.        Awe Na sifa zote za mwanachama wa kawaida.
ii.      Awe mwanachama Kwa muda wa miaka mitatu (2) mfululizo isipokuwa viongozi wa kwanza kuchaguliwa baada ya usajili wa katiba hii hawatafungwa na sharti hili la muda.
iii.     Asiwe amepatikana na hatia ya kosa lolote la jinai. iv.Awe na taaluma ya uhasibu.

SEHEMU YA V1: MAJUKUMU YA VIONGOZI


IBARA YA 20:  KAZI ZA MWENYEKITI
i.          Kuwajibika kwenye mkutano mkuu kuhusu maswala yote ya kiutendaji ya kikundi.
ii.         Kuitisha vikao vya Kamati Kuu na vya Mkutano mkuu kwa kufuata Kalenda ya mikutano ya Kikundi.
iii.       Kuongoza vikao na mikutano yote ya kikundi ambayo yeye ni mjumbe.
iv.       Kusimamia utekelezaji wa maamuzi yanayotolewa na kikundi
v.        Kutia saini katika hundi na nyaraka mbali mbali za kitendaji kwa mujibu wa Katiba vi.Kuwa msemaji mkuu wa kikundi.
vii.         Kuwa na kura ya turufu katika maamuzi ambapo pande mbili zinapolingana.
viii.        Kusaini mikataba na makubaliano kati ya kikundi na taasisi nyingine au watu binafsi kama itakavyokubaliwa ndani ya vikao vinavyohusika ikiwa itahitajika hivyo na kanuni.

IBARA YA 21: KAZI ZA KATIBU WA KIKUNDI

i.    Kuratibu shughuli zote za kikundi.
ii.  Kukusanya taarifa za kila kikao, kutoa taarifa kwa wanakikundi. iii. Kuweka kumbukumbu na nyaraka zote za kikundi.
iii.   Kwa kushirikiana na Kamati Tendaji kuandaa  Mikutano ya Kikundi.

IBARA YA 22: KAZI ZA MWEKA HAZINA

i.        Kupokea fedha zote zinazoingia katika kikundi, kuweka kumbukumbu na kuzihifadhi fedha benki au kadiri ya maelekezo ya kamati kuu au mkutano wa kikundi.
ii.      Kutoa risiti kwa fedha zote atakazopokea na kutunza nakala; na kupokea na kutunza stakabadhi kwa malipo yote anayofanya.
iii.     Kuandaa taarifa za mapato na matumizi ya kikundi kwa kila robo mwaka.  iv.Kuwasilisha taarifa ya mapato na matumizi kwenye vikao husika au itakapohitajika.
v.    Kujibu hoja za wakaguzi wa hesabu.
vi.  Kutia saini kwenye hundi. vii.Kuratibu masuala yote yanayohusu fedha  na mahesabu ya kikundi.
viii.Kutoa taarifa ya madeni ya Wanakikundi angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu.

SEHEMU YA VII: UCHAGUZI NA MUDA WA KUKAA MADARAKANI IBARA YA 23: MUDA WA UONGOZI

23.1 Viongozi wote katika kikundi watashika nafasi zao kwa muda wa miaka mitatu.
23.2 Kiongozi anaweza kuchaguliwa zaidi ya vipindi viwili katika nafasi moja.  Anaweza kuchaguliwa tena kama ameshakaa nje ya uongozi kwa kipindi kimoja lakini anaweza kuchaguliwa katika nafasi nyingine mara baada ya ukomo wa uongozi wake wa vipindi vya miaka mitatu.
23.3 Uchaguzi Mkuu utafanyika kila baada ya miaka mitatu. Na Kamati Kuu itaandaa kanuni za uchaguzi.
23.4Uchaguzi mdogo unaweza kufanyika iwapo;
i.          Kiongozi au Viongozi fulani watashindwa kuongoza kwa ajili ya kuhamishwa kikazi,
ii.         Ikiwa kiongozi atapata ugonjwa utakaomfanya ashindwe  kuendelea na  majukumu yake,
iii.       Kifo au;
iv.       kuondolewa kwa mujibu wa katiba.
23.5. Nafasi ya Uongozi ikiwa wazi itajazwa katika Mkutano Mkuu unaofuata
23.6. Katika kipindi cha mpito Kamati kuu itakuwa na mamlaka ya uteuzi wa mtu miongoni mwa wanakikundi atakayekaimu nafasi iliyoachwa wazi.

SEHEMU YA VIII: MIKUTANO YA KAWAIDA NA YA DHARURA

IBARA YA 24: MKUTANO MKUU
24.1 .Mkutano Mkuu: Kitakuwa chombo chenye maamuzi ya juu na ya mwisho katika uendeshaji wa kikundi na  shughuli zake.
24.2 .Utaongozwa na mwenyekiti wa kikundi na kuratibiwa na katibu wake ikiwa mwenyekiti hayupo kitaongozwa na Makamu Mwenyekiti na ikiwa Makamu Mwenyekiti hayupo, kitaongozwa na mjumbe atakayechaguliwa na mkutano husika kuongoza mkutano mkuu huo.
24.3 .Mkutano mkuu utaitishwa na Mwenyekiti wa kikundi  kwa kutoa  notisi ya siku ishirini na moja ikiwa ni pamoja na kuwapelekea wanakikundi agenda za mkutano huo husika.
24.4 .Mwanakikundi anaweza kumteua mwanakikundi mwenzake kumwakilisha kwenye mkutano mkuu (PROXY) kwa kujaza fomu maalum au njia nyingine kadiri itakavyoamuliwa na miongozo mingine ya kikundi. Mwanakikundi anayemwakilisha mwanakikundi mwenzake ataweza kupiga kura kwa niaba ya mwanakikundi anayemwakilisha. Mwanakikundi hataruhusiwa kuwakilisha zaidi ya wanakikundi wa tatu (3) katika kikao kimoja.
24.5 .Mkutano mkuu utafanyika mara mbili kwa mwaka. Kila mkutano mkuu utapanga tarehe ya mkutano mkuu unaofuata isipokuwa kipindi cha mkutano mkuu mmoja na mwingine hakitazidi miezi sita (6). Kwa kuepuka mashaka mkutano mkuu wa kwanza wa kikatiba utafanyika Jumapili. Wajumbe wa Mkutano Mkuu ni wanachama wote wa kikundi cha ASILI YETU.
24.6.Ikiwa kwa sababu yoyote  itaonekana  haitawezekana  kufanyika Mkutano Mkuu  katika tarehe zilizopangwa, Kamati Kuu itakuwa na mamlaka ya kubadili tarehe  ya mkutano mkuu, lakini mkutano huo usiwe  zaidi ya mwezi mmoja kabla au baada ya tarehe  iliyotajwa.
24.7. Akidi ya mkutano mkuu ni moja ya tatu (theluthi moja) ya wanakikundi walio na uanachama hai.

IBARA YA 25:  KAMATI MBALI MBALI

25.1 KAMATI KUU

Kutakuwepo na Kamati Kuu. Itakayo ratibu shughuli zote za kikundi Na kusimamia kamati mbalimbali. Kama hizi zita wajibika chini ya wakuu wake
25.2. Kamati Kuu itakuwa na wajumbe wafuatao;
i.                        Mwenyekiti.
ii.                      Makamu wa’’
iii.                       Katibu.
iv.                       Katibu Msaidizi.
v.                      Mweka Hazina.
vi.                    Wenyeviti wa kamati zote.
vii.                   vii.Wajumbe wanne watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu.

25.3. KAMATI YA FEDHA NA UWEKEZAJI

25.3.1 Kutakuwepo na kamati ya Miradi.  Ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao;
i.          Mwenyekiti atakayeteuliwa na Kamati Kuu.
ii.         Katibu atakayeteuliwa na Kamati Kuu.
iii.       Wajumbe wanne (4) watakaoteuliwa na Kamati Kuu.

25.4  KAMATI YA SHUGHULI ZA KIJAMII

25.4.1 Kutakuwepo na Kamati ya Shughuli za Kijamii.  Ambayo wajumbe wake watakuwa;
i.          Mwenyekiti atakayeteuliwa na Kamati Kuu.
ii.         Katibu atakayeteuliwa na Kamati Kuu.
iii.       Wajumbe wane
iv.       watakaoteuliwa na Kamati Kuu.

25.5 KAMATI YA MAADILI NA MARIDHIANO

25.5.1 Kutakuwepo na kamati ya Maadili, Nidhamu na Maridhiano  ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao;
i.          Mwenyekiti atakayeteuliwa na Kamati Kuu.
ii.         Katibu atakayeteuliwa na Kamati Kuu.
iii.       Wajumbe wanne (4) watakaoteuliwa na Kamati Kuu

25.6 KAMATI YA KATIBA NA KANUNI

25.6.1 Kutakuwepo na Kamati ya Katiba na Kanuni  ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao;
i.          Mwenyekiti atakayeteuliwa Na Kamati Kuu.
ii.         Katibu atakayeteuliwa Na Kamati Kuu.
iii.       Wajumbe wanne (4) watakaoteuliwa Na Kamati Kuu.

25.7 KAMATI YA TEHAMA

25.7.1 Kutakuwepo Na Kamati ya Tehama itakuwa Na wajumbe wawili watakaoteuliwa Na Kamati Kuu
IBARA YA 26:  MAJUKUMU YA KAMATI

26.0 KAZI ZA MKUTANO MKUU

26.1 Mkutano Mkuu ndio utakuwa na madaraka ya mwisho katika kikundi.
26.2 Mkutano Mkuu utachagua viongozi wafuatao;
i.               Mwenyekiti wa Kikundi
ii.              Makamu Mwenyekiti wa Kikundi
iii.            Katibu wa Kikundi
iv.            Katibu Msaidizi wa Kikundi
v.             Mweka Hazina wa Kikundi
vi.            Wajumbe wanne wa Kamati Kuu wa kikundi ambao ni, utaidhinisha uteuzi wa viongozi na wanachama wapya na maamuzi mengine muhimu yahusuyo shughuli za kikundi.
26.3 Wajumbe waliochaguliwa katika ibara (vi) watakuwa wajumbe wa kamati kuu pamoja na wenyeviti wa kamati.
26.4 Utapokea na kupitisha taarifa za fedha, miradi na shughuli za kijamii za kikundi.
Kusimamia uongozi ili utekeleze maazimio ya mkutano mkuu.
26.5 Kuamua watia sahihi wa chama kwenye mikataba na  akaunti za benki.
26.6 Kuamua na kuthibitisha wakaguzi wa nje wa hesabu za miradi ya kikundi kadiri itakavyohitajika.
26.7 Kupokea, kujadili na hatimaye kuidhinisha mpango kazi wa mwaka wa fedha unaoanza wa kikundi kadiri utakavyowasilishwa na kamati kuu ya kikundi.
26.8 Kuidhinisha mkopo au vyanzo vingine vya fedha kwa ajili ya miradi ya kikundi kadiri itakavyohitajika.

26.8.8 KAZI ZA KAMATI KUU

8.8.1 Kuandaa agenda za Mkutano Mkuu
8.8.2 Kusimamia utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa na Mkutano mkuu
8.8.3 Kuwasilisha mahesabu ya fedha za kikundi kwenye Mkutano Mkuu
8.8.4 Kuratibu shughuli na utendaji wa kikundi
8.8.5 Kujadili maombi ya wanaotaka kujiunga na kikundi na kuangalia mienendo ya wanakikundi.
8.8.6 Kubuni mbinu za kuongeza ufanisi katika uendeshaji.
8.8.7 Kuunda kamati ndogo na kuitisha vikao au mikutano ya dharura pale inabopidi.
8.8.8 Kupendekeza mkaguzi wa hesabu wa Kikundi.
8.8.9 Kamati ya Kuu  itakuwa na mamlaka ya kutunga kanuni na taratibu za  Kikundi na kisha kuziwasilisha  katika Mkutano Mkuu kwa ajili ya kupitishwa. Kanuni na taratibu za utekelezaji zilizotungwa au zitakazotungwa  kuongoza shughuli mbalimbali za kikundi hiki ni kama zifuatavyo;
i.      Kanuni za kusajili wanachama wapya.
ii.     Kanuni za Utendaji kazi za Uongozi.
iv.                Kanuni za Uchaguzi.
v.                 Kanuni za ukusanyaji wa udhibiti wa mali za Kikundi.
v.             Kamati ya utendaji inaweza kupendekeza kwenye Mkutano Mkuu.
vi.           Kanuni nyingine za utendaji wa Kikundi.

26.8.9    KAZI ZA KAMATI YA FEDHA NA UWEKEZAJI

8.9.1 Kusimamia uendeshaji wa  shughuli zote za miradi mbali mbali ya kikundi
8.9.2 Kusimamia utekelezaji wa  sera zinazoongoza miradi
8.9.3 Kupeleka mapendekezo ya kiutendaji kwa Kamati Kuu kwa maamuzi zaidi.
8.9.4 Kubuni miradi  na mbinu bora za kuimarisha na kulinda miradi.
8.9.3 Kutoa taarifa za miradi kwenye mkutano mkuu.
8.9.4 Kuandaa  utaratibu wa ajira endapo itahitajika kuajiri wafanyakazi kwenye  miradi ya  kikundi na kuufikisha utaratibu huo mbele ya mkutano mkuu kwa  kuridhiwa.
8.9.5 Kufanya kazi nyingine yoyote itakayopangiwa na  Mkutano Mkuu.

26.9.1 KAZI ZA KAMATI YA SHUGHULI ZA KIJAMII

9.1.0 Kuratibu shughuli zote za maafa na sherehe kuzingatia taratibu.
9.1.1 Kubuni, kupendekeza na kuratibu mahusiano na shughuli mbalimbli kati ya kikundi na taasisi nyingine pamoja na jamii.

26.9.2 KAZI ZA KAMATI YA MAADILI NA MARIDHIANO

9.2.1  Kupatanisha wanakikundi pale inapotokea kutokuelewana.
9.2.2  Kupokea mashauri yote ya kinidhamu yanayohusu mwanakikundi na kikundi                    ambayo yanaweza kupelekea kusitishwa kwa uanakikundi wa mwanakikundi.
9.2.3  Kutoa taarifa ya maswala ya kinidhamu na mahusiano kwenye kamati kuu na                   mkutano mkuu. Kupanga na kuratibu maswala yanayohusu maadili na mambo ya                  kiroho yanayohusu kikundi pamoja ustawi wa kikundi.

26.9.3 KAZI ZA KAMATI YA KATIBA NA KANUNI

9.3.1 Kushauri  Kamati Kuu kuhusu mambo yote ya kisheria  yanayohusika na Kikundi.
9.3.3 Kushirikiana na kamati  mbalimbali katika  kutengeneza kanuni za kikundi kwa    kadiri ya mahitaji.
9.3.4    Kusaidia  kusaidia kamati ya maadili ikiwa  kamati hiyo itahitaji ujuzi wa kikanuni              au kisheria  kutoka kwa  wataalamu wa sheria.
9.3.5 Kutoa ushauri wa jumla kwa kikundi  katika kuhakikisha kikundi  kinatekeleza        shughuli zake kwa mujibu  wa katiba yake, kanuni na sheria za nchi.


26.9.4 KAZI ZA KAMATI YA TEHAMA

9.4.1  Kushauri Kamati Kuu kuhusu mambo yote ya TEHAMA ambayo  Kamati Kuu                     itahitaji kuyafahamu katika ufanyaji maamuzi.
9.4.2          Kutoa mapendekezo mbalimbali kwa Kikundi  au kamati za kikundi ya namna                           bora ya kutumia TEHAMA katika  kuboresha shughuli za kikundi.
9.4.3  Kufanya kazi nyingine yoyote inayohusiana na TEHAMA kama itakavyoagizwa                     na Kikundi au kamati zake.

IBARA YA 27: MIKUTANO YA DHARURA
27.0  Wanakikundi wanaweza kuitisha Mkutano wa dharura kujadili jambo                   linaloonekana kuwa la haraka na lazima kushughulikiwa na kikundi
27.1 Ili kuitisha  mkutano wa dharura itatakiwa  wanachama wanaozidi nusu  ya             wanachama hai wote waweke sahihi kwenye pendekezo lililotayarishwa na      mwanachama au wanachama wanaotaka  kuitisha mkutano huo wa dharura.
27.2  Baada ya wanachama zaidi ya nusu kuweka sahihi zao kwenye pendekezo la       kuitishwa kwa mkutano wa dharura,  pendekezo hilo litawasilishwa kwa katibu   ambaye      ataanza mchakato wa kuhakikisha mkutano wa dharura unaitishwa  kama   ulivyopendekeza.

SEHEMU YA IX: VIKAO NA MKUTANO

IBARA YA 28: UTARATIBU WA VIKAO NA MKUTANO

28.1  Bila kuathiri  maelezo ya ibara ya 4.1.2 ya Katiba hii, Mkutano Mkuu wa
Kikundi utafanyika kila Jumapili ya kwanza ya mwezi Februari na kila Jumapili ya             kwanza baada ya sikukuu ya Mt. Francisco.
28.2  Vikao vya Kamati Kuu vitafanyika angalau kila baada ya miezi mitatu.
28.3   Vikao vya Kamati za miradi na shughuli za kijamii vitafanyika angalau mara             moja kwa miezi mitatu.
28.4  Mikutano na vikao vinaweza kufanyika zaidi pale itakapohitajika.
28.4.0 AKIDI
28.4.1    Ili mkutano au kikao chochote kifanyike, lazima idadi ya wajumbe ifikie zaidi ya              nusu ya wajumbe wote walio hai.
28.4.2     Kila suala la kawaida kiutendaji litaamuliwa na wengi, mwenyekiti atakuwa na                kura ya turufu endapo itatokea  kura zinashindwa kupata uamuzi wa                  wengi.Maamuzi yanayohusu kubadili ibara  ya katiba hii au kumvua mtu     uanachama   yatafikiwa  ikiwa tu  idadi ya kura  inafikia theluthi mbili ya     wajumbe wote waliopiga kura.

SEHEMU YA X: UTUNZAJI WA FEDHA,VYANZO VYA FEDHA NA MATUMIZI YA FEDHA ZA KIKUNDI


IBARA YA 29:MAPATO NA MATUMIZI

Mapato  ya kikundi yatatokana na  vyanzo vifuatavo;
i.Ada ya kiingilio  kama itakavyopitishwa na mkutano  mkuu.
ii.Michango ya Ada ya kila mwezi kama itakavyokubaliwa na mkutano  mkuu. iii.Faini mbalimbali kama zitakavyopitishwa na kanuni.
iv.Faida zitokanazo na miradi mbalimbali ya kikundi
IBARA YA 30: VYANZO VYA FEDHA
30.1 Kutakuwa na vyanzo vya fedha za kikundi kama ifuatavyo;
i.          Ada za kujiunga za wanakikundi
ii.         Ada za kila mwezi za wanakikundi
iii.       Penati mbalimbali kama itakavyo amuliwa katika mkutano mkuu
iv.       Vyanzo vingine vitokanavyo na riba, faida katika miradi ya kikundi

IBARA YA 31: MATUMIZI YA FEDHA

31.1 SHUGHULI ZA KIJAMII- SHEREHE
Mkutano Mkuu wa kikundi utaamua aina ya shughuli  ambazo  kikundi kitahusika kwa  kutoa mchango wake kama kikundi au  kwa wanakikundi kuchangia. Maamuzi ya kikao      yatadumu hadi yatakapobadilishwa na  maamuzi ya kikao kingine .
31.2. SHUGHULI ZA KIJAMII- MAAFA/ MATATIZO
Mwanakikundi, mwenzi na wategemezi wake watastahili kuhudumiwa kama ifuatavyo;
i.          Watoto wasioidi wanne ambao amewaainisha katika fomu
ii.         Wazazi wa mwanakikundi.
iii.       Wategemezi wasiozidi wanne walioainishwa na mwanakikundi.
31.3UGONJWA
Mwanakikundi, mwenzi au mtegemezi atasaidiwa kadiri ya kanuni zitakazowekwa na     Kikundi.
31.4 MISIBA
Mwanakikundi akifariki, familia yake itapewa rambirambi kutoka fedha za kikundi kama  itakavyopendekezwa na kamati kuu na kuamuliwa na mkutano mkuu. Pia familia itapewa  fedha zitokanazo na hisa na akiba zake kwenye miradi aliyoshiriki, endapo zitakuwepo  itakavyokuwa imeamuliwa na kikundi. Endapo mwanakikundi atafiwa  na mke, mtoto,  mzazi au wategemezi waliotajwa katika taarifa za mwanakikundi kwa mujibu wa kanuni  za Kikundi. Mwanakikundi atapewa rambirambi kwa  kiwango kitakachopendekzwa na  kamati kuu na kupitishwa na mkutano  mkuu.

IBARA YA 32: UENDESHAJI WA AKAUNTI ZA BENKI ZA KIKUNDI

32.0  Kwa mujibu wa Ibara hii Kikundi kitakuwa na akaunti ya benki itakayo simamiwa na        Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, katibu na Mhazini wa Kikundi au itakavyo kuwa    imeelekezwa na Mkutano mkuu.

IBARA YA 33: TAARIFA YA FEDHA YA MWAKA

33.0 Kwa mujibu wa ibara hii taarifa ya fedha itatolewa katika Mkutano mkuu utakao fanyika    kwa mujibu wa katiba hii. Kamati Kuu itasimamia utoaji wa ripoti za kila baada ya Miezi  mitatu mitatu kulingana na ratiba ya vikao vya kamati hiyo kwa uongozi wa Kikundi.

IBARA YA 34: UDHIBITI NA UKAGUZI WA FEDHA

34.0 Kutakuwa na ukaguzi wa hesabu za Kikundi kama mkutano Mkuu utakavyo kuwa            umeamua.

IBARA YA 35: USIMAMIZI WA KIKUNDI

35.0  Kikundi kitakuwa na USIMAMIZI NA ULEZI wa watu na wadau muhimu kama itavoamuliwa na Mkutano mkuu
35.1  Kikundi kitakuwa na mlezi atakayeteuliwa na Kamati Kuu na kuthibitishwa na mkutano  mkuu wa kikundi. Atakuwa ni mshauri wa maswala yote ya kikundi.



SEHEMU YA XI: MABADILIKO YA KATIBA, MALI ZA KIKUNDI NA KUVUNJA KIKUNDI

IBARA YA 36: MABADILIKO YA KATIBA

36.1 Katiba hii inaweza kubadilishwa sehemu yake, au vipengele vyake au kuongezwa ibara mpya au kufutwa ibara iliyopo au kuifanyia marekebisho katiba yote na Mkutano Mkuu wa Wanakikundi kwa kura zisizopungua asilimia 75 ya wanakikundi hai (bila PROXY) walioshiriki katika mkutano mkuu.
36.2 Mwanakikundi yeyote anayetaka kufanyia mabadiliko katiba hii au sehemu ya katiba hii atatakiwa kutoa taarifa ya maandishi kwa katibu ambaye ataisambaza kwa wanachama walau si chini ya miezi miwili kabla ya mkutano husika ikionyesha aina ya mabadiliko yanayopendekezwa.
36.3 Mkutano mkuu unaweza kuyakubali mabadiliko yanayopendekezwa au kuyafanyia maboresho mabadiliko hayo au kuyakataa.

IBARA YA 37: MALI ZA KIKUNDI

37.1 Mali zote za Kikundi zitakuwa chini ya jina la kikundi na zitakuwa chini ya              uongozi wa Kikundi.
37.2 Uongozi wa kikundi  utatunza kumbukumbu za mali zinazomilikwa na kikundi         kwa kadiri ya utaratibu utakaowekwa.
37.3  Mali, jina au nembo ya kikundi vitatumika TU kwa namna iliyoidhinishwa na
Kikundi
37.4  Mkutano mkuu wa  pili wa  kikundi  utachagua na kupitisha jina la Mkaguzi wa  Hesabu    za kikundi. Hesabu za kikundi zitakaguliwa kila mwaka.

IBARA YA 38: KUVUNJIKA KWA KIKUNDI

38.1 Kikundi hiki kinaweza kufutwa ikiwa sheria za nchi zinalazimu kikundi kifutwe
38.2 Kikundi pia kinaweza kufutwa endapo asilimia 75 ya wanakikundi hai wataridhia                hivyo katika mkutano mkuu.
38.3 Endapo kikundi kitafutwa fedha na mali zote za miradi na uwekezaji zitatumika                   kwanza  kulipia madeni ya kikundi yaliyopo  kwa mujibu wa sheria za nchi  na  kulipia  gharama za ufilisi na endapo  kutakuwepo salio zitarudishwa kwa wanakikundi kufuatana na uwiano wa hisa wanazomiliki.



SEHEMU YA XII: MENGINEYO

IBARA YA 39: UTATUZI WA MIGOGORO

Kwa mujibu wa ibara hii kikundi kita tumia njia ya maridhiano ya ndani ya kikundi.
Na endapo pale mgogoro utavuka hatua hii kikundi kita husisha walezi na wasimamizi wa kikundi.
Bila kuathiri malengo ya kikundi na kanuni zake migogoro yote itamalizwa kwa kanuni za maadili na utendaji zitakazo kuwa zimeundwa na Kamati Kuu kwa Mujibu wa Katiba hii.